Home KITAIFA COMRADE KINANA AIPONGEZA UWT KWA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NCHINI

COMRADE KINANA AIPONGEZA UWT KWA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NCHINI

Na Mwandishi wetu, Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara COMRADE Abdulrahman Kinana ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoa mafunzo ya mara kwa mara yanayolenga kujenga uwezo kwa Viongozi na Watendaji Wanawake nchini.

Comrade Kinana ametoa pongezi hizo leo Mei 25, 2024 akifungua mafunzo ya Wanawake wanasiasa yaliyoandaliwa na UWT Jijini Dodoma.

Washiriki wa mafunzo hayo ni Wabunge wanawake wa CCM wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Watendaji wanawake wa CCM kutoka jumuiya ya wazazi,Wenyeviti wa CCM Wanawake wa Mikoa na Wilaya.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT )Taifa, Mary Chatanda MCC, Katibu Mkuu wa UWT, Suzan Kunambi (MNEC).

Huo ni Muendelezo wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi wa Viongozi na Watendaji Wanawake nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here