Home KITAIFA NAWASHUKURU KWA DUA ZENU – DK.MWINYI

NAWASHUKURU KWA DUA ZENU – DK.MWINYI

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Wazee wa Vijiji vya Ukongoroni na Charawe kwa kumuombea dua baada ya kukamilika barabara ya Ukongoroni hadi Charawe na kuipongeza Serikali.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa na dua ya kumuombea iliyoandaliwa na Wazee wa Ukongoroni na Charawe iliyofanyika Ukongoroni, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Mei, 24 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea dua nchi ili Mwenyezi Mungu aidumishe katika amani na kutimiza ahadi za maendeleo kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here