Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA IRAN NCHINI

RAIS DK.SAMIA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA IRAN NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania kufuatia Kifo cha Rais wa Nchi hiyo Hayati Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya Helikopta nchini Iran. Rais Samia alisaini Kitabu hicho katika Ubalozi wa Iran uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam Mei, 24 2024. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Hossein Alvandi Bahineh.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini, Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam Mei, 24 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam Mei, 24 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Hossein Alvandi Bahineh pamoja na Maafisa Mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam Mei, 24 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here