Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital
IMEELEZWA kuwa dunia ya leo inayobadilika kwa kasi ni budi kutengeneza rasilimali kupitia ubunifu ili kusaidia kubadili changamoto na kuwa fursa kwani karne ya 21, zinazochagizwa zaidi na mapinduzi ya teknolojia, utandawazi, na mandhari yanayobadilika ya kijamii na kiuchumi, mahitaji ya nguvu kazi yenye ujuzi inayoweza kubadilika zaidi kuliko hapo awali.
Akizungumza Mei 20 jijini Dar es Salaam Wahariri na Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Amos Nungu , wakati akifafanua juu ya Wiki ya Ubunifu Tanzania toleo la kumi linalotarajiwa kuzinduliwa hapo Kesho 21 Mei 2024 Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam na Kilele chake kufanyikia Mkoani Tanga.
Amebainisha kuwa huo ni mwanzo wa wiki ya Ubunifu ambapo kesho Ukumbi wa Mwalimu Nyerere itazinduliwa rasmi na kilele kitakiwa ni Tanga wiki ijayo hivyo amewaalika wabunifu wote kuhudhuria kwani kutakuwa na mijadala mbalimbali itakayozungumzwa na kazi za kibunifu huku wakiongozwana Kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa maendeleo kwa maendeleo Jumuishi ya Rasilimali watu”.
Jukwaa hilo litaleta mijadala yenye tija na kuleta pamoja Makundi mbalimbali ya kibunifu kuchangia katika kuleta elimu, ujuzi na Ubunifu. Wiki ya ubunifu imekuwepo kwa Miaka 10 Mfululizo. Lengo ni kiwa na Ubunifu wa kiuchumi shindani.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema ni heshima kubwa kualikwa kuwa sehemu ya Kongamano hili la Vyombo vya Habari kuelekea Wiki ya Ubunifu Tanzania 2024 na ametoa shukrani kwa waandaaji, COSTECH na Mradi wa Ubunifu wa FUNGUO chini ya UNDP Tanzania, kwa kumualika ili kushiriki mawazo juu ya mada muhimu ya “Kukidhi Mahitaji ya Rasilimali Watu ya Sasa na Ya Baadaye kupitia Mfumo wa Elimu unaoendana na wakati.”
“Ningependa kutambua washirika wetu wa maendeleo, Umoja wa Ulaya, FCDO, na UNDP ambao wanaendelea kuchangia katika jitihada zetu za maendeleo na wamefanikisha mpango wa FUNGUO. Pia naelewa kuwa tuna idadi ya washirika wengine ambao wamekuwa wakiiunga mkono jukwaa la Wiki ya Ubunifu, ikiwa ni pamoja na UNICEF, UNWOMEN, ENABEL, VODACOM, na wengine,”amesema Profesa Nombo.
Ameeleza kuwa Tanzania, kama mataifa mengine mengi, inakabiliwa na changamoto ya kuoanisha mfumo wake wa elimu na mahitaji yanayobadilika ya sasa na ya baadaye. wanatambua kuwa njia moja kwa wote katika elimu haiwezekani tena, badala yake, wanapaswa kuunda mfumo wa elimu unaokuza vipaji mbalimbali, unachochea ubunifu, na kuandaa kizazi chenye ujuzi na umahiri unaohitajika kustawi katika dunia inayobadilika kwa kasi.
Kwa mfano, nyote mnajua kuwa sasa tuna sera mpya ya elimu na tumetangaza mtaala mpya, unaoweka mkazo mkubwa katika kukuza ujuzi unaofaa kwa soko la ajira linalobadilika, kama vile fikra tunduizi, utatuzi wa migogoro, mawasiliano, na ujuzi wa kidijitali.
Aidha Taifa halina budi kuangalia mbele, ushirikiano itakuwa muhimu kufanya kazi pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali – ikiwa ni pamoja na serikali, vyuo vikuu, sekta ya viwanda, vyombo vya Habari, na jamii – kuja na suluhisho zinazoshughulikia mahitaji yanayobadilika ya rasilimali watu wetu. Kwa kukuza ushirikiano na kutumia utaalamu wa pamoja na rasilimali za wadau wote, tunaweza kuunda mfumo wa elimu ambao unaendana ipasavyo kwa mahitaji ya karne ya 21.