Home BURUDANI HARMONIZE ANATARAJIA KUZINDUA ALBUM YA TANO MEI 25

HARMONIZE ANATARAJIA KUZINDUA ALBUM YA TANO MEI 25

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

MSANII wa mziki bongo fleva Rajab Abdul maarufu kama “Harmonize” Mei 25,2024 anatarajia kuzindua album yake ya tano ambayo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia.

Uzinduzi huo utakaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam’ akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Dk.Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na (kurefresh) huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

Amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku pekee sana kwa watanzani kutakuwa na mialiko na hakutakuwa na viingilio

“Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Dk.Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here