Home KITAIFA WATANZANIA 32000 WANAPOTEZA MAISHA HAWATUMII NISHATI SAFI

WATANZANIA 32000 WANAPOTEZA MAISHA HAWATUMII NISHATI SAFI

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

WAZIRI Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jafo amesema takwimu zinaonesha takribani ya watanzania 32000 kila mwaka wanapoteza maisha kwa sababu hawatumii nishati safi.

Akizungumza Mei 17,2024 na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Paris Nchini Ufaransa Mei,14 mwaka huu ambapo Rais Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alikuwa Kinara na Mwenyekiti Mwenza katika mkutano huo wa Kimataifa.

“Afrika sasa watu milioni 900 wanahangaika na nishati safi ya kupikia na takwimu zinaonyesha sisi Tanzaniani takribani 32000 kila mwaka wanapoteza maisha kutona na matumizi ya nishati isiyokuwa salama kupikia,”amesema Dk.Jafo.

Amesema mkutano uliofanyika Paris nchini Ufaransa hamasa yake kubwa imetoka kwetu watanzania ambaye Rais Dk.Samia katika mkutano wa mwaka jana wa Tabianchi ilikuwa chanzo kikubwa cha kuchagiza mkutano huo Rais amewaheshimisha kwa sababu wote waliokuja pale ajenda ilikuwa ya Tanzania.

Dk.Jafo amesema hekta laki 46942 n uharibifu wa mazingira kila mwaka hiyo ni changamoto kubwa ni kweli lipo wazi ilik kuondokana na changamoto hiyo lazima wahakikishe kupunguza uharibifu wa mazingira kuondoka huku na kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia.

“Ili kutumiza malengo kufikia mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia lazima wapate elimu ni muhimu kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya nishati safi,” amesema.

Akizungumza Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Wizara hiyo inaendelea kutekeleza agizo la Rais Dk.Samia la kuleta pamoja wadau na wabunifu ili kusaidia watanzania kutumia gesi ya kupikia kwa kulipia kuanzia shilingi elfu moja hadi 10,000 na kuendelea kulingana na matumizi yake kama ilivyo kwenye luku za umeme.

Amesema umuhimu wa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwaajili ya kuepuka kuhatarisha uharibifu wa mazingira ndani ya nchi na nje kwa ujumla.

“Kuboresha teknolojia mbalimbali za nishati safi ya kupikia kwa sababu sio LPG peke yake au gesi peke yake zipo teknolojia nyingi tukitaka kupunguza gharama ni lazima kuwekeza kwenye bunifu mbalimbali,”amesema Kapinga.

Amefafanua kuwa wanaendelea Kuboresha miundombinu ya umeme ili watanzania wengi wakipata umeme wa uhakika watumie majiko ya umeme yaliyoboreshwa na pressure cooker unatumia chini ya unit moja kuchemsha maharage kwa muda mfupi.

“Tunaendelea kuhamasisha tuwe wabunifu wa teknolojia nyingine za nishati safi ya kupikia ili kupunguza gharama wapo wadau tumeanza kuwaleta pamoja ili kuhakikisha tuna teknolojia nzuri mfano M Gas wao wanateknolojia yao unaweza kununua gesi kiasa chochote unataka kuanzia elfu 1,000, 2,000 ,3,000, 5,000 na hili inawezekana, ” amesema.

Ameongeza kuwa elimu bado inahitajika mfano Dar es Salaam ni mjini lakini wanaongoza kwa matumizi ya mkaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus amesema malengo ya mkutano huo kuipa kipaumbele nishati safi ya kupikia anga za kimataifa japo lilikuwa linahusisha nchi za Afrika.

Amesema ajenda za mkutano huo ni paomoja kuwepo na sera kwasababu nchi nyingi hazina sera ya nishati safi ya kupikia na walikuwa kushawishi kuwepo na sera nchi mbalimbali na kuharakisha ushirikiano wa wadau mbalimbali.

“Taasisi ya Nishati ya Kimataifa (IIE) inakadikiliwa kuwa na uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 4 zitahitajika kila mwaka barani Afrika ili wote waweze kuwa na nishati safi ya kupikia ifikapo 2030,”amesema Zuhura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here