Home KITAIFA ZANZIBAR NA COMORO ZINA MAHUSIANO MAALUM

ZANZIBAR NA COMORO ZINA MAHUSIANO MAALUM

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Ofisi ya Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar Mei 14 2024.

Pia amemtaka Balozi Yakubu kuangalia fursa zilizopo za kuuza bidhaa mbalimbali kutoka nchini na kuzisimamia hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano wa kudumu ikiwemo katika sekta ya afya, elimu, utamaduni, biashara, usafirishaji na habari kupitia shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC).

Aidha amesema Shirika la Meli la Zanzibar lina mpango wa kuagiza meli mbili mpya, ameleeza pia MV.Mapinduzi imeshafanyiwa ukarabati na hivi karibuni itaanza safari zake kutoka Zanzibar kwenda Comoro.

Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar imejipanga kwa utalii wa matibabu kwa kuifanya hospitali mpya ya Lumumba kuwa kituo cha kupokea wagonjwa kutoka nje hasa nchi ya Comoro pindi itakapokamilika na kuanza kutoa huduma.

Naye Balozi Yakubu amemuahidi Rais Dk.Mwinyi kudumisha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Zanzibar na Comoro pamoja na kuendeleza hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano ya kudumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here