Home KITAIFA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA UNICEF-MAJALIWA

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA UNICEF-MAJALIWA

Na Mwandishi wetu Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Elke Wisch, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu amemuahidi Wisch kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kulipa ushirikiano Shirika hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, maji na elimu.

Kwa upande wake, Wisch ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mipango katika kuboresha sekta ya elimu, mpango wa kukabiliana na maafa pamoja na kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha, Wisch ameahidi shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuandaa na kutekeleza mpango kazi wa kukabiliana na maafa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here