Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam , Albert Chalamila leo Mei 13, 2024 amekabidhi Mwenge wa Uhuru 2024 Mkoa wa kusini Pemba-Zanzibar
Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam ulipokelewa Mei 8, 2024 ukitokea Mkoa wa Pwani ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umekimbiza Mwenge wa Uhuru katika umbali wa kilometa 427.78 kwa kupitia miradi 39 yenye thamani ya shilingi 479,649,649,667 miradi ambayo baadhi ilikuwa imekamilika, na mingine katika hatua za utekelezaji
Aidha katika Wilaya zote tano za Mkoa huo Mbio za Mwenge wa Uhuru, zimetembelea, zimekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru 2024 hakuna mradi uliokataliwa
Vile vile Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo zimeelimisha na kuhamasisha wananchi kupitia Ujumbe wa ” Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”
Pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa
Pia Wilaya ya Ubungo ndio imehitimisha mzunguko wa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo ambapo Chalamila alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko katika viwanja vya Barafu mburahati mapema leo