Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA KUHUTUBIA JUKWAA LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA AFRIKA

RAIS DK.SAMIA KUHUTUBIA JUKWAA LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA AFRIKA

Na Esther Mnyika @Lajiji Digital

RAIS  Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kushiriki katika mkutano wa kilele cha wakuu wa nchi kuhusu nishati safi ya kupikia duniani, Paris nchini Ufaransa.

AkizungumzaLeo Mei, 11 2024 na waandishi wa habari, Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba, alisema Dk. Samia ataanza ziara hiyo  leo Mei 12 hadi 15, nchini humo,  ambapo atakuwa  Mwenyekiti mwenza wa kuongoza mkutano huo.

Pia Makamba amesema katika ziara hiyo, Rais Dk. Samia atakutana na kufanya mazungumzo na  Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron kuimarisha uhusiano wa kirafiki na kihistoria katika huduma za afya, elimu kupitia mfuko wa misaada wa Ufaransa.

“Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi barani Afrika na baadhi ya nchi za Ulaya na tayari watu 900 wameshajiandikisha kushiriki katika mkutano huo uliondaliwa na taasisi ya nishati duniani, Serikali ya Ufaransa, Tanzania  na Benki ya Maendeleo ya Afrika”, amesema.

Makamba amesema lengo la mkutano huo ni  kuifanya nishati safi ya kupikia kuwa kipaumbele katika agenda za kimataifa kupate wadau wengi zaidi.

Pia kuainisha hatua madhubuti za kisera zinazoweza kuharakisha matumizi ya nishati safi za kupikia na kutoa fursa kwa washiriki kutoa ahadi za kifedha ahadi za mabadiliko ya sheria na kisera pamoja na ubia katika adhima kukuza nishati safi ya kupikia.

Aidha Makamba amesema faida ya ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo ni kuonyesha fursa ya nchi imepiga hatua kuliko nchi nyingi duniani na kuweka sera mikakati na mipango zaidi ya matumizi ya nishati hiyo.

Amesema washiriki wa mkutano huo ni Wakuu wa nchi Barani Afrika, baadhi ya nchi za Ulaya pamoja na watu wengi mashuhuri duniani wakiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani (WHO) na viongozi wanaomaliza muda wake wa COPE 28 na ajae.

Mkutano huo utagawanywa katika majopo matatu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza jopo la pili lenye mada kufanya nishati ya kupikia ni kipaumbele barani Afrika.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here