Home KITAIFA WAZIRI KUVALIA NJUGA MIGOGORO YA ARDHI SAME.

WAZIRI KUVALIA NJUGA MIGOGORO YA ARDHI SAME.

Ashrack Miraji, Same

WAZIRI wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa amekubali kuambatana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharib, David Mathayo mara baada ya kumaliza kuwasilisha bajeti ya wizara yake mwezi june mwaka huu ili kwenda kutatua migogoro ya Ardhi inayoendelea katika katika Jimbo lake Mkoani Kilimanjaro.

Ametoa kauli hiyo baada ya kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo hilo aliyetaka kujua lini Waziri huyo atakwenda kutatua kero na migogoro ya aridhi Inayoendelea katika Kijiji Cha Bangalala tarafa ya mwembe- Mbango kata ya Makaya na Ruvu katika wilaya ya Same ambayo inapelekea kukwamisha maendeleo ya wananchi hasa katika kipindi hichi Cha kilimo na ufugaji.

Aidha Waziri Silaa ameomba radhi kwa wananchi wa Same hasa wa jimbo la Same Magharibi ambao January 26 mwaka huu alitembelea sehemu ya migogoro hiyo kata ya Bangalala Makanya na Ruvu na pia akatuma watahalam kwenda kupima maeneo na mipaka na tayari ameshawasilishiwa ofisini, hivyo baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge ataongozana na Mbuge David Mathayo kwenda kuitatua.

Awali Mathayo amesema migogoro hiyo imedumu kwa zaidi ya miaka 19 bila ya ufumbuzi wowote na kupelekea Wananchi kutoelewana na kusimamisha shughuli za maendeleo katika maeneo hayo pamoja na kuishi kwa amani na upendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here