Na Mwandishi wetu, Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakub, aliyekwenda kumuaga ofisini kwake leo Mei 9, 2024 Jijini Dodoma.
Dk. Biteko amempongeza Balozi Yakub kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kuiwakilisha Tanzania katika Visiwa vya Comoro.
Aidha, amemuasa kutumia vyema nafasi hiyo kwa Taifa, hasa kwa kuainisha maeneo ya kimkakati ambayo yatawezesha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za uchumi na maendeleo ya kijamii.
Kwa upande wake Balozi Yakub amemshukuru Naibu Waziri Mkuu na kuahidi kuongeza fursa mbalimbali kwa Watanzania Visiwani humo.