Home KITAIFA SIMBACHAWENE AWASILI IRINGA KUTETA NA WATUNZA NYARAKA NA KUMBUKUMBU.

SIMBACHAWENE AWASILI IRINGA KUTETA NA WATUNZA NYARAKA NA KUMBUKUMBU.

Na Mwandishi wetu, Iringa

MKUU wa wilaya ya Iringa, Kheri James mapema leo amempokea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora George Simbachawene alie wasili wilayani Iringa kwa jukumu la kuhudhuria kikao kazi cha Taasisi ya watunza nyaraka na kumbukumbu TRAMPA.

Pamoja na mambo mengine Waziri atafanya jukumu la kufunga kikao kazi hicho kilichofanyika kwa siku tatu kwa lengo la kujengeana uwezo na kukumbushana misingi ya maadili ya taaluma hiyo na majukumu yake.

Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika kikao hicho, Mkuu wa wilaya hiyo, James amewapongeza viongozi na wanachama wa TRAMPA kwa kufanikiwa kufanya mkutano huo muhimu na amewashukuru kwa kuchagua kufanyia mkutano huo mkoani Iringa, hatua ambayo imesaidia kuchangia uchumi wa wana Iringa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here