Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro amefanya kikao na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini Mei, 8, 2024 Jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine wamejadili maendeleo ya mchezo huo, akiwataka kuheshimu taratibu, miongozo pamoja na Katiba za vyama vinavyounda Kamisheni hiyo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Gerson Msigwa, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Ally Mayay na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha.