Na Nihifadhi Issa, zanzibar
JUMLA ya wanafunzi laki mbili hufanya maombi ya masomo kupitia Taasisi ya Teknolojia ya India (IIT MADRAS) kwa kila mwaka.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Dhamana wa Taasisi hiyo Profesa. Preeti Aghalayam alipozungumza na wanafunzi wa kidato cha tano na kidato cha sita wa Skuli ya Sekondari ya Biashara unguja.
Akitoa wasilisho kwa wanafunzi hao Profesa. Preeti amesema kwa ujumla wake wake IIT Madras ni taasisi inayowavutia wanafunzi wengi kuhitaji kujiunga kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na mitaala yake ya kimataifa na idadi ya vitivo vya fani mbali mbali za
kimasomo zinazotolewa na IIT Madras.
Ameongezea na kutaja sababu hizo kwa kusema kuwa, ushikirikiano wa karibu wa wahitimu, uwepo wa klabu za kimafunzo za kitaalamu na kuendelea kushikilia ubora wa utaoji wa elimu
wa masuala ya kiteknolojia ni sababu nyengine muhimu zinazochangia uhitaji wa kujiunga na IIT Madras.
Ametaja kuwa, IIT Madras imeweka mazingira mazuri kwa kila mhitaji aweze kushiriki na kujiunga na masomo yawe ya juu, mbali na ratiba za kujisomea masuala ya kijamii pia yanazingatiwa.
Wakitoa maoni yao katika mkutano huo wanafunzi wa ZANCOM wameipongeza IIT Madras kwa hatua zake za kuanza usaili mapema na kuahidi kuitumia nafasi hiyo kutuma maombi yao kama ilivyoelekezwa.
Jumla wa wanafunzi 100 walihudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mkutano wa Skuli ya Sekondari ya Biashara (ZANCOM).