Home KITAIFA DK.KIJAJI ATAKA WADAU KUJIPANGA NA TEKNOLOJIA AKILI MNEMBA

DK.KIJAJI ATAKA WADAU KUJIPANGA NA TEKNOLOJIA AKILI MNEMBA

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, DK.Ashantu Kijaji ametoa wito kwa wadau wote husika kujipanga kama Taifa ili kunufaika fursa zinazotokana na teknolojia ya akili mnemba

Akisoma hotuba leo Machi 15 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri huyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Hashil Abdallah wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya mlaji duniani ambayo huadhimishwa machi 15 kila mwaka yaliyoandaliwa na TumeyaUshindani Nchini (FCC).

Amesema kuhimarisha Matumizi ya serikali mtandao na kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kiteknolojia katika utendaji wa taasisi za umma ikiwa pamoja na matumizi ya akili mnemba ili kufikisha na kuridhisha huduma kwa wadau.

“Ili kujadili dhana ya akili mnemba na jinsi gani mlaji anapaswa kulindwa dhidi ya changamoto mbalimbali zinaweza kusababishwa na teknolojia hiyo,Jambo hili ni la kupongezwa kwa kuwa duniani ndio inakoelekea na Tanzania inabidi kuwa tayari kukabiliana na Teknolojia hiyo kwa kuwa nchi yetu sii kisima,”amesema.

Amesema matumizi ya akili mnemba katika utoaji huduma kwa walaji ni dhana mpya ambayo kwa sasa imeshika. kasi. duniani kote.

Ameeleza kuwa ni eneo jipya ambalo. linakua kwa kasi hivyo ni jambo muhimu kwa vyombo usimamizi wa vyombo vya utendaji wa uchumi wa soko vinavyotoa huduma kwa wananchi ni jukumu la FCC pamoja na taasisi nyingine zinazoshughulika na biashara.

Dk. Kijaji amesema mifumo ya akili mnemba ni dhahili kwani imekuwa ikitumika sehemu mbalimbali kurahisisha huduma ikiwemo huduma ya usafirishaji.

“Kulingana na uzoefu wa kimataifa kama ilivyoelezwa na taasisi Huru ya kutetea walaji duniani Ili kuwezesha kupatikana kwa udhibiti na uhakika wa matumizi ya akili mnemba Katika kutoa huduma kwa walaji unazingatia uwajibikaji jaki na maslai yao kwa ujumla,” amesema

Ameongeza kuwa maeneo yafuatayo lazima yawe kipaombele katika utekelezaji wa eneo hilo l msingi la kumlinda mlaji katika uchumi wa soko nchini.

Amesema eno la kwanza uundwaji wa mifumo ya huduma inatumia akili mnemba walaji wana hofu kuhusu namna ambavyo mfumo akili mnemba inavyoundwa

Amefafanua kuwa mifumo hiyo kwa kiasi kikubwa uhitaji taarifa nyingi katika kufanikisha uundwaji na utendaji wake hivyo wanapaswa kuhoji na kutafiti namna ambavyo mifumo hiyo inaundwa na kusimamiwa na endapo hayo yatafanyika kwa namna inayolinda maslahi ya mlaji hivyo ni dhahhiri itasaidia kufikia malengo.

Aidha amesema kubainishana faida na athari za akili mnemba matumizi ya akili mnemba katika huduma za mlaji ili kuwezesha kutunga sera, Sheria mifumo ya usimamizi na udhibiti pamoja na watafiti

Ameongeza kuwa serikali kupitia Mamlaka zake wataendelea kuweka utaratibu wa kudhibiti utakao wataka watoa huduma wanao tumia mifumo ya teknolojia hizo kuweka bayana changamoto zinazoweza kujitokeza kwa walaji kutumia teknolojia hiyo na kutatua na njia bora ya kuelimisha jamii kutokana na changamoto hizo ili kuwa makini wanapotumia teknolojia hiyo.

Dk. Kijaji amesema ni muhimu kwa washirika wa kongamano hilo kujadiliana kwa kina ili kujenga ufumbuzi wa pamoja kwa changamoto zinazoletwa na ukuaji wa Sayansi na teknolojia katika kusambaza bidhaa na huduma na jinsi ya kumlinda mlaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio amesema ni ahadi ya baraza kwamba wataendelea kushirikiana na Mamlaka za udhibiti pamoja na FCC katika kuhakikisha kwamba wanaendeleza sheria za ushindani, udhibiti na kumlinda mteja.

Amesema lengo kubwa la sheria za ushindani sio tu kuwalinda washindani bali kumlinda mlaji hivyo, pale wanapoona sheria hizo zinashindwa kumlinda mlaji ipasavyo wanayo fursa kuzibadilisha ili kuendana na hali ambayo ipo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania( CTI ), Mhandisi Leodger Tenga amesema elimu waliyotoka nayo kwenye mkutano huo watakwenda kuwashirikisha wenye viwanda kwani kuna mengi mapya wameyaona.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dk. Eliezer Feleshi alizungumzia umuhimu wa kuhakikisha kunakuwepo na sheria ambazo zitawaleta katika ulimwengu sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema lazima pia, kuwe na mifumo ya kidigitali inayoongelea FCC na ZFCC katika ulindaji wa haki.

Amesema inahitajika bajeti ya kutosha kuwezesha FCC na ZFCC kufanya shughuli zake kwa urahisi kwani maeneo ya walaji haki zao zinaendana na tafiti na matokeo ya kila siku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here