Home KITAIFA CHADEMA WAMESHIRIKI KIKAMILIFU MCHAKATO WA KUTUNGA SHERIA MPYA YA UCHAGUZI

CHADEMA WAMESHIRIKI KIKAMILIFU MCHAKATO WA KUTUNGA SHERIA MPYA YA UCHAGUZI

Na Mwandishi wetu, Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesema CHADEMA wameshirikishwa a kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutungwa sheria mpya ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM jijini Dodoma leo Mei, 5, 204, Kinana amesema CHADEMA imetoa maoni kupitia makundi matatu tofauti maoni yao kuzingatiwa.

“Kwa kawaida wadau hutoa maoni bungeni kwa siku moja, lakini ili kutoa nafasi kwa wadau katika sheria hii (sheria ya uchaguzi) Bunge lilitoa nafasi kwa siku nne ili watu wengi washiriki kutoa maoni.

“CHADEMA wlipeleka makundi yote, walikwenda kama chama, walikwenda kama BAVICHA (Baraza la Vijana CHADEMA) na walikwenda kama BAWACHA (Baraza la Wanawake CHADEMA) lakini bado hawaridhiki,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here