Home KITAIFA BENOITE AMEWAOMBA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI KUENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI...

BENOITE AMEWAOMBA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI KUENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Na Esther Mnyika, @Lajiji Digital

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania, Benoite Araman amewaomba waandishi habari na wahariri kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umma ili kuhakikisha lengo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati hiyo ili kulinda afya zao na mazingira.

Wito huo ametoa leo April 30,2024 Jijini Dar es salaam wakati ya hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na jiko lake kwa waandishi wa habari na wahariri iliyofanyika katika ‘Depot’ ya gasi iliyopo Kigamboni .

“Tunaahidi kama ilivyokuwa siku zote tutaendelea na kampeni hii kadri ya uwezo wetu ili kuhakikisha tunaunga mkono kwa vitendo jitahada za Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha anamsaidia mwananchi hasa mwanamke kumtua kuni kichwani na kulinda afya yake na mazingira,” amesema Benoite.

Amesema Oryx wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo adhama hiyo ya Rais kwani mpaka sasa wameshagawa mitungi ya gesi 33000 kwenye maeneo mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Ametaja faida za kutumia gesi ya Oryx amesema matumizi ya gesi kwenye taasisi yanasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi hiyo kutafuta nishati mbadala kama kuni na mkaa.

Amesema kupikia kwenye gesi hiyo kunalinda afya na mazingira na kutokomeza ukatiji wa misitu na kunamsaidia kulinda afya mwanamke ambao wanaathirika kwa moshi unaotokana na mkaa na kuni.

“Kutumia gesi hii kunalinda mazingira kwa kutunza misitu kwani misitu hiyo ni muhimu kwa viumbe hai,kuhifadhi udongo,kusaidia mzunguko wa maji lakini pia kulinda ekolojia na rasilimali za asili.

“Wanawake wanaathirika kwa kutumia kuni na mkaa kwani moshi unachembechembe za sumu ambazo husababisha magonjwa kama pneumonia,cancer ya mapafu na matatizo ya upumuaji,”amesema.

Ametaja sababu nyingine ya kutumia gesi hiyo pia ni kupunguza ukatili unaowapata wanawake na watoto pindi wanapoenda kutafuta kuni misitu pia kuepuka kujeruhiwa na wanyama wakali hivyo kwa kufanya hivyo itawaokolea muda na kuweza kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Nishati Safi ya wa Oryx, Peter Ndomba amesema wameendelea kutoa hamasa na elimu kwa wananchi kutunza fedha kidogo kidogo ili pindi gesi inapoisha waweze kujaza lakini pia wameshaongea na benki ya TPB kuweza kusaidia wananchi kupeleka pesa kidogo kidogo kwa ajili ya kununulia gesi pindi inapoisha.

Aidha amesema 2021 walikua na mradi wa kijiji hadi kijiji ili kuhakikisha wanakuwa na wasambazi ambapo baada ya hapo waliingia zoezi la nyumba hadi nyumba ili kuhakikisha nishati hiyo inaweza kumfikia kila mwananchi na kuachana na kutumia nishati chafu.

“Tanzania inanyumba takribani milioni 14 na kati hiyo ni milion mbili tu ndio zinatumia na sisi lengo letu kuhakikisha angalau nyumba milioni 8 zinatumia nishati hii ya Oryx,”mesema Ndomba.

Ameongeza kuwa mitungi yao ya gesi ni salama na imewekwa alama zote za usalama pindi mtumiaji anapotumia anaweza kuzitumia taratibu hizo ili kuendelea kuwa salama lakini pia wanaendelea kutoa elimu mara kwa mara ya namna bora na salama ya kutumia mitungi hiyo.

Amesema wamekuwa wakigawa mitungi ya gesi na majiko kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na mama lishe watumishi wa sekta ya afya na wajasiliamali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here