Home KITAIFA WAMI RUVU HAWANA DENI LA RAIS SAMIA KATIKA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI.

WAMI RUVU HAWANA DENI LA RAIS SAMIA KATIKA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI.

Na Mwandishi wetu,Morogoro

BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu limeendelea kuchukua hatua stahiki katika kuhakikisha inatekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philipo Isory Mpango la kupanda miti 2,000,000 kwa kila mkoa ikiwa ni mkakati wa uhifadhi wa Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji katika bwawa la Mindu.

Wakati Akikagua leo Aprili, 27eneo la mradi wa uhifadhi wa mazingira katika bwawa la Mindu lililopo Manispaa ya Morogoro linalosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Eliakumu Mnzava amepongeza hatua madhubuti zinazochukiwa na Bonde katika kutunza vyanzo vya maji kwa kuendelea kuhamasisha zoezi la upandaji wa miti ambapo mpaka sasa takribani miti elfu 24,255 imekwisha pandwa katika mradi huo.

“Hata kwa kuangalia inaonesha watu wapo serious (Makini) kwenye upandaji wa miti katika chanzo hiki cha maji, Lakini pia tumepata wasaa wa kuona miti iliyopandwa katika Mwenge wa uhuru 2023 na namna ambavyo inaendelea, mlipanda miti 2,000 na miti 1939 inaendelea vizuri, Wenzetu wa Wami wanaendelea kurudishia miti 61 ambayo imekufa, hii kazi mmeifanya vizuri sana kwenye eneo la utunzani wa mazingira na upandaji miti, wenzetu wa Wami Ruvu hatuwadai chochote,” amesema Mnzava.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Rebeca Nsemwa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Manispaa ya Morogoro na kikosi cha Jeshi la Mzinga kwa kuungana na serikali katika ulinzi na utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji, ambapo hadi sasa miti 76,926 ilipandwa katika maeneo ya shule, Hifadhi ya Milima Uruguru, Bwawa la Mindu pamoja na eneo la Jeshi Magadu.

Mradi wa uhifadhi wa Mazingira katika Bwawa la Mindu umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 50,000,000 ambazo ni michango ya miche na nguvu kazi ya jamii ikiwa na lengo la kulinda chanzo hiko cha maji kinachotegemewa na kwa zaidi ya asilimia 70% na wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here