Home KITAIFA FCS yapongeza miaka mitatu ya Rais Dk.Samia ukuaji wa demokrasia

FCS yapongeza miaka mitatu ya Rais Dk.Samia ukuaji wa demokrasia

Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Asasi za Kiraia Nchini (FCS )anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga, amesema Shirika hilo linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya demokrasia.

Akizungumza jana Machi 5 jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya uongozi kati yake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge aliyechaguliwa hivi karibuni.

Amesema kuwa FCS inajivunia uongozi wa Rais Samia unaoheshimu misingi ya democrasia na uhuru wa watu, ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

“Kwetu sisi tunaona ni taasisi inayopigania misingi ya utawala bora, tunahitaji kuendeleza juhudi za kupambania maendeleo ya watu, na hili ni suala la kujikumbusha kila siku” amesema Kiwanga.

Ameongeza licha ya kuwa anamaliza muda wake amehahidi kuendeleza ushiriano na Shirika hilo na atakuwa balozi kwa kutoa mchango wake pindi atakapohitajika.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya FCS, DK. Ally Laay, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake kwa kuwa mchapakazi, mwadilifu na kusimamia majukumu yake kwa weledi na kuiheshimisha FCS.

Aidha, amesema kuwa ana imani kubwa na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake Mei mosi, 2024.

“Bwana Rutenge ameshinda kwa kishido kikubwa licha ya kuwepo ushindani mkubwa katika mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya, bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea aliposhia kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana” amesema Laay.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS, Justice Rutenge ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here