Dar es Salaam
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kuanzia Mei mosi 2025 itasitisha rasmi matumizi ya Namba ya Utambulisho wa Taifa (NINs) zao ambao waliotumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) hawakujitokeza kuchukua Vitambulisho vyao.

Pia imesisitiza kwamba yule ambaye matumizi ya NINs yatafungwa hatoweza kuitumia namba hiyo kwaajili ya huduma yeyote.
Tangazo hilo limetolewa leo Aprili, 14 2025 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA,James Kaji amesema dhamira yao na serikali kwa ujumla ni kuona kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na mhusika na hasa ikizingatiwa serikali imetumia fedha nyingi kutengeneza.
“Hataweza kuitumia tena baada ya kwenda kuchukua kitambulisho chake naomba ieleweke kwamba hujapokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) unaokutaka kwenda kuchukua kitambulisho chako namba yako haitafungwa.
Kwa kuzingatia kuwa tulikwishatuma sms kwa watu karibu wote ambao vitambulisho vyao vilikusanywa toka serikali za vijiji, Mitaa, Vitongoji,Kata na Shehia na kwa kuwa tuliwatangazia kwamba tutafunga matumizi ya NINs kwa wale wote ambao tumekwisha zalisha Vitambulisho vyao na kuwatumia sms ya kuvifuata lakini bila sababu yeyote ile ya msingi hawakujitokeza kuichukua,” amesema Kaji.
Amesema wanalazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kwamba waliwatumia njia mbalimbali kuwafahamisha na kuwahamasisha wananchi kuchukua vitambulisho vyao tangu walipovipeleka katika ofisi za Kata, Vijiji, Mitaa, na Shehia.
“Uamuzi wetu huu wa awali wa kuvipeleka huku ulifanywa kwa dhamira njema ya kuwaondolea usumbufu wananchi wa kuvifuata katika ofisi za NIDA za Wilaya ili badala yake wavichukue huku katika maeneo ambayo ni karibu na makazi yao,” amesema.
Kaji akizungumzia kuhusu zoezi la kukusanyaji vitambulisho na kutuma sms alisema tangu kuanza kwa zoezi hilo kuanzia mwezi Januari hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya wananchi 1,88060 sawa na asilimia 157 ya watu wote walikuwa hawajachukua vitambulisho vyao licha ya kutumiwa ujumbe mfupi (sms).
“Kwa mujibu wa takwimu hizi idadi ya wananchi waliojitokeza kuchukua vitambulisho baada ya kupokea sms ni 565,876 sawa na asilimia 30 tu ya watu wote waliotumiwa na kupokea sms,”amesema.
Aidha amesema NIDA imeaandaa mpango wa usajili na utambuzi wa watu wote wenye umri chini ya miaka 18 kuwezesha upatikanaji wa Jamii Namba pamoja na wageni wote wanaoingia nchini na kukaa chini ya miezi sita.
Ameeleza kuwa itakumbukwa kwa sasa wageni wanaosajiliwa, kutambuliwa na kupewa jamii namba ni wale wanaokaa nchini kwa zaidi ya miezi sitana kibali cha makaazi.
Kaji amefafanua kuwa mpango huo wa usajili wa watu wenye umri chini ya miaka 18 utaanza kwa majaribio katika Wilaya tatu ambazo ni Kusini_Kusini Unguja, Kilolo na Rungwe ambapo wanatarajia kusajili jumla ya watu 235,826 ndani ya miezi miwili.