Home BIASHARA TCB NA RAMANI.IO WAMEZINDUA RASMI USHIRIKIANO WA KULETA MAGEUZI KATIKA...

TCB NA RAMANI.IO WAMEZINDUA RASMI USHIRIKIANO WA KULETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA BIASHARA

Dar es Salaam

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Ramani.io wamezindua rasmi ushirikiano unaolenga kuimarisha biashara za ndani na kuongeza ujumuishaji wa kifedha nchini wakilenga kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya biashara, ikiwemo kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), wajasiriamali, pamoja na biashara ndogondogo.

Akizungumza leo Aprili, 9 jijini Dar es salaam wakati wa kutia hati ya Makubaliano (MoU) inayoweka msingi wa ushirikiano huo wa kimkakati, Afisa Mkuu wa Digitali na Ubunifu TCB, Jesse Jackson amesema Benki hiyo inaamini katika kujenga ushirikiano.

Amesema ushirikiano huo na Ramani.io utawasaidia kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi kwa urahisi na haraka na pia kuwasaidia kukua kwa pamoja na kujenga uchumi wa nchi.

“Hii ni hatua muhimu katika kuongeza upatika wa wahudumu za fedha kwa wajasiriamali na biashara ndogo ndogo na inatarajiwa kuwa na athari kubwa katik kukuza uchumi,” amesema.

Amesema Lengo kuu ni kuleta urahisi katika shughuli za fedha, kuongeza ufanisi wa uendeshaji na kukuza biashara zao kwa njia endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji (CEO) na Mwanzilishi Mwenza wa Ramani,Lain Usiri amesema kuwa ushirikiano huo kati ya TCB na Ramani io unaweka kiwango kipya cha ubunifu na ushirikiano katika sekta ya kifedha

“Mfano wa kuigwa wa namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kukuza biashara za ndani lakini pia ni uthibitisho wa wazi wa dhamira ya pamoja ya kuendeleza uchumi jumuishi na endelevu nchini Tanzania,” amesema.

Ameongez kuwa kupitia ushirikiano huo changamoto katika mnyororo wa ugavi na usambazaji zitashughulikiwa kwa kutumia teknolojia bunifu ya Ramani.io sambamba na huduma bora za kifedha kutoka TCB yenye mtandao mpana kuongeza,Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara kupata mitaji kwa urahisi, kuongeza ufanisi wa uendeshaji, na kukuza biashara zao kwa njia endelevu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here