Pwani
BANDARI Kavu ya Kwala inahudumia kontena 823 kwa siku na kwa mwaka 300000 zikiwemo zinazokwenda nchi jirani ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya kontena zinazohudumiwa Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo ameyabainisha leo Machi, 16 2025 Mkoani Pwani na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea mradi wa kongani ya viwanda vya mkoa huo pamoja na Bandari ya Kwala iliyojengwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
Ameeleza kuwa bandari hiyo na zingine zinazojengwa Mwanza, Isaka, Tabora na mipakani mwa nchi za Burundi, Rwanda,Congo DRC kutapunguza msongamano wa shehena Bandari ya Dar es Salaam.
“Hili eno la kwala peke yake linaweza kuhudumia makontena 300000 kwa mwaka bandari yetu ya Dar es Salaam ni kama mara tatu yake lakini tayari tushaanza kuona baada ya kuchukua hatua mbalimbali za kuiboresha bandari ishaanza kuzidiwa nadhani tukitumia hapa na bandari zetu zingine tulizozijenga Dom na Tabora na Mwanza zitataua changamoto ya msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam itakuwa imekwisha,” amesema Msugwa.

Amesema Sababu za kuleta bandari hiyo hapo ni kwamba wamejenga eneo hilo la kwala ambalo liko karibu na barabara kuu ya Dar es Salaam na Morogoro lakini jirani kabisa na reli ambayo iko jirani.
Amefafanua kuwa wamejenga bandari hiyo kwa ajili ya kukabiliana na msongamano katika bandari ya Dar es Salaam sasa katika bandari hiyo kulikuwa na ICD bandari kavu ndogondogo kama 11 zile bandari zimeshindwa kuhimili mizigo makontena mengi ambayo yanaletwa uwezo wake ilikuwa ni kuhifadhi makontena 24300 kwa wakati mmoja sasa licha ya hivyo pia kulikuwa na bandari kavu za magari kama 9 zenye uwezo wa kuhifadhi magari kama 19100.
“Katika utekelezaji wa mradi katika eneo hili tupo awamu ya kwanza, na tutaendelea kufanya katika maendeleo mengine mpaka tufikie hekta zote ambazo tumeziandaa katika eneo hili lengo ni kwamba tuwe na eneo ambalo linavutia na ambalo wawekezaji wakija hawatapata changamoto ya kuchukua ama kuhifadhi mizigo yao,” ameongeza.
Amesema inamrahisishia mtu yeyote ambaye mzigo wake unakuja hapo na kuamua kutoa hapo ama kwa kutumia reli au barabara.
Aidha Msigwa amesema zaidi ya vijana 1000 wameajiriwa katika kiwanda cha San Ton Park kilichopo eneo hilo kinachozalisha bidhaa kama majokofu, nguo na vifaa vingine.
“Sekta ya viwanda imeleta mapinduzi chanya kiuchumi, huku mapato yake yamefukia shilingi trilioni 2 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na ajira zaidi ya laki tano zimeongezeka kupitia miradi mbalimbali ya viwanda,” amesema.