Home KITAIFA RAIS DK. MWINYI: SERIKALI ITAZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA KIJAMII.

RAIS DK. MWINYI: SERIKALI ITAZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA KIJAMII.

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewahakikishia Wananchi wa Mpapa kuwa Serikali itazifanyia kazi changamoto za kijamii ziliomo katika kijiji hicho.

Alhaji Dk.Mwinyi ametoa Tamko hilo leo Machi, 14 2025 alipotoa Salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kujumuika katika sala ya ijumaa, Msikiti wa Ijumaa Mpapa, Wilaya ya Kati ,Mkoa wa Kusini Unguja.

Changamoto hizo zilizobainishwa na Wananchi ni uchakavu wa barabara za ndani , ukosefu wa uzio katika Skuli ya Mpapa na ukosefu wa huduma za Karibu za afya kutokana na kutomalizika kwa kituo cha afya kiliopo kwa miaka mingi ambacho kimejengwa kwa nguvu za wananchi.

Rais Dk. Mwinyi amewahakikishia kuwa Serikali itamaliza changamoto hizo alizoziielezea kuwa ni za muhimu.

Pi amewasisitiza waumini hao kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na viongozi wakuu wa nchi.

Amefafanua kuwa maendeleo yanayofikiwa hivi sasa hapa nchini yanatokana na kuwepo kwa amani na kuahidi kuendeleza juhudi za kuleta maendeleo Zaidi.

Wakati huohuo Rais Dk. Mwinyi alikikagua Kituo hicho cha afya ambacho hakijamalizika kwa takribani miaka 30 tangu kilipojengwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here