Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI: SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDONBINU YA SEKTA YA ELIMU

RAIS DK.MWINYI: SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDONBINU YA SEKTA YA ELIMU

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itaendelea kuimarisha miundonbinu ya sekta ya elimu kwani ndio kipaumbele cha kwanza cha serikali anayoiongoza.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo leo Machi, 12 2025 wakati wa Ufunguzi wa Skuli Tatu Mpya za Msingi za Ghorofa za Chumbuni, Kidichi na Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume iliopo Mwera.

amefafanua kuwa serikali inajikita kuimarisha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya msingi , sekondari na vyuo vikuu kwani ni nyenzo Mlmuhimu ya kufanikisha maendeleo katika sekta zote.

Amebainisha kuwa kwa Muda mrefu Zanzibar ilikuwa ikikabiliana na changamoto tatu kuu katika sekta ya elimu ambazo serikali imeamua kuziondosha.

“Changamoto hizi ni pamoja na ukosefu wa miundonbinu ya elimu iliobora, upungufu wa walimu hususani wa masomo ya sayansi pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunza ambazo kwa kiwango kikubwa zilidhorotesha maendeleo ya elimu hapa nchini,” amesema.

Dk.Mwinyi ameeleza kuwa serikali itaendelea na Uujenzi wa Slskuli za ghorofa katika maeneo mbalimbali pamoja na Kuongeza Idadi ya walimu sambamba na kuimarisha maslahi yao ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha amefafanua kuwa serikali inakusudia kuzifanya skuli zote kuwa na viwango bora vya kujifunzia kwa kuwa na vifaa vya kutosha vya kujifunzia, maabara, maktaba na vyumba vya kompyuta Ili kuwaandaa wanafunzi katika ngazi za awali.

Pia ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa usimamizi nora wa ujenzi wa skuli hizo tatu pamoja na uongozi wa wilaya na mikoa kwa ufuatiliaji wa miradi hiyo.

Rais Dk. Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa kamwe hatayumbishwa na kauli potofu za elwatu wasiopenda maendeleo katika dhamira yake ya Kuleta maendeleo na mabadiliko katika sekta ya elimu.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa amesema Mageuzi Makubwa yanayoendelea katika Sekta ya Elimu yanasaidia Kuongeza Ufanisi katika Utekelezaji wa Mtaala Mpya wa Elimu na Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi.

Akiwasilisha taarifa ya kitaaluma ya ujenzi wa skuli hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla amesema kila Skuli imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5 hadi kukamilika zikiwa na madarasa 29 kila moja , maabara, maktaba na vyumba vya kompyuta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here