Home KITAIFA CHALAMILA AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA PROFESA SARUNGI

CHALAMILA AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA PROFESA SARUNGI

Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Machi 10, 2025 ameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyewahi kuwa waziri na Mbunge wa Rorya Profesa Philemon Sarungi katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila akitoa Salaam za Mkoa ametoa rai kwa jamii kujenga tabia ya kusema mazuri ya mtu akiwa hai kuliko kutoa sifa nyingi akiwa ameaga Dunia ambapo anakuwa hawezi tena kutambua chochote.

Vilevile ametoa salaam za Pole kwa familia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ambapo amesema Dk. Nchimbi amemtuma awape pole nyingi familia, ameshindwa kuja kutokana na muingiliano wa ratiba na ameahidi kufika nyumbani kuwafariji.

Aidha Profesa Sarungi mwenye umri wa miaka 89 alifariki Dunia Jioni ya Jumatano Machi 5, 2025 nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam kwa tatizo la Moyo, mwili wake unatarajiwa kuzikwa leo Machi 10, 2025 katika makaburi ya Kondo Kunduchi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here