Na Esther Mnyika, Arusha
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga kizazi Chenye maadili mema ya kitanzania na kuheshimiana ili kuwe na jamii bora itakayozaa taifa imara.

Hayo ameyasema leo Machi, 8 2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Kitaifa iliyofanyika Viwanja vya Michezo vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha amesema umuhimu wa kulea watoto wanaojiamini na wenye uwezo wa kujenga Howard badala ya kuwa na vijana wasiojiamini na wenye kupaza sauti bila ya kuwa na hoja zenye kueleweka.
Amesema na sio jukumu la Serikali, mwalimu na mzazi katika malezi bora ya mtoto ni wajibu wa kila mmoja kwa manufaa ya nchi.
“Vijana kujitambua ndiyo mambo pekee ambayo yanaweza kufanikisha malengo na ndoto za Tanzania za kuwa na taifa jumuishi lenye ustawi na haki ambalo litakwenda kinyume na ubaguzi mbalimbali. Katika ngazi ya jamii,” amesema Dk.Samia.

Rais Dk. Samia akizungumzia kuhusu Mabadiliko ya sera na sheria kukuza usawa kwenye jamii amesema Serikali itaendelea kufanya mabadiliko mbalimbali ya Sera na sheria ili kuleta mabadiliko mbalimbali kwenye katika kuimarisha usawa na haki.
Amesema pamoja na mengine mabadiliko hayo ni katika kuwafanya Wanawak kuweza kumiliki ardhi. Pamoja na ujumuishi wa huduma za afya kwa kuwezesha Bima kwa wote katika kudhibiti na kulinda hadhi zilizofikiwa kama taifa.
“Serikali itaendelea kuimarisha huduma nyingine za kijamii ikiwemo utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa kushughulikia kasoro mbalimbali za kimfumo na kusimamia kikamilifu mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo sasa inawezesha watanzania wasiokuwepo kwenye ajira rasmi kuweza kunufaika na mifuko hiyo,”amesema.

Ameongeza kuwa umuhimu wa kuwa na Serikali inayoamini katika usawa wa kijinsia huku akiwataka wanawake na sekta mbalimbali. Kuhamasisha jamii kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kuendelea kusimamia usawa wa kijinsia.
Dk.Samia amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kufanikishamalengo ya kuhakikisha kesho bora na njema zaidi kwa vijana wa kitanzania wa kike na kiume na inajivunia mengi katika kuboresha mazingira yanayohakikisha ndoto ya usawa wa kijinsia inafanikiwa.

“Tunapo adhimisha miaka 30 tangu Tamko la Umoja wa Mataifa la Mkutano wa Beijing miaka 10 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia na miaka mitano ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ni fursa ya Kutathmini mafanikoa makubwa yaliyofikiwa na kutambua hatua zaidi zinazohitajika ili kuhakikisha kila msicha na mwanamke hapa nchini anapata nafasi ya kufikia ndoto zake,” ameeleza.
Rais Dk. Samia ametaja hatua kubwa zilizochukuliwa katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini sambamba na malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa alisema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza umaskini, kukomesha njaa kuboresha afya na ustawi, elimu bora usawa wa kijinsia, maji safi na usafi, nishati mbadala, kuimarisha amani, haki na taasisi madhubuti.
Kwa upande wa umasikini wamepunguza asilimia 26 kutoka kiwango cha awali walipoanza utekelezaji wa na dira na uhakika wa chakula Tanzania inajitegemea chakula kwa asilimia 128 imefanikiwa kuondoa njaa asilimia 100.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi amewaomba wanawake kuwa sehemu ya kutunza Amani ya nchi.
“Leo niseme basi kinamama tunawaomba amani ya nchi ipo mikononi mweni hivyo msichoke kutufundisha, kutukumbusha na kutumemea kila mtakapoona tunahatarisha amani ya nchi yetu,” amesema Dk.Nchimbi.

Awali akizungumza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum, Dk.Dorothy Gwajima amesema mwaka huu wanawake wameitika kwa kushiriki makongamano ya wanawake yaliyofanyika sehemu mbalimbali nchini.

“Hii Indonesia kuwa wanawake wameiitika hatutakuwa na makongamano ya kuongea ongea tulikuwa tunafanya maonesho ya bidhaa zilizozalishwa na wanawake wajasiriamali na kutoa huduma,”amesema.