Home KITAIFA VETA KUADHIMISHA MIAKA 30 NA 50 YA ELIMU YA UFUNDI

VETA KUADHIMISHA MIAKA 30 NA 50 YA ELIMU YA UFUNDI

Dar es Salaam

MAADHIMISHO ya miaka 50 ya Mfumo wa Kitaifa wa Serikali ya Taasisi ya Kusimamia Ufundi Stadi pamoja na miaka 30 ya Mamlaka ya elimu na mafunzo ufundi stadi (VETA) yanatarajia kufanyika Machi 18 hadi 21 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hayo yamebainishwa leo Machi, 5 2025 jijini Dar es salaam na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema maadhimisho hayo yamekuja baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kutaka kukamilisha vyuo vya veta kila mkoa.

“Kwa sasa tupo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha chuo Songwe huku vyuo 64 vikiendelea na ujenzi wake lengo ni kuhakikisha kila kijana wa Kitanzania anapata elimu ya ufundi stadi,”amesema.

Aidha amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanywa na wanafunzi wao ikiwemo kupaka rangi majengo ya shule na kuonyesha bunifu zao mbalimbali zinazofanywa .

Profesa Mkenda amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali kuelekea Kilele cha maazimisho hayo ambazo ni
pamoja na kutoa huduma kwa jamii zinazoendana na shughuli za ufundi na ufundi stadi.

Amesema shughuli nyingine ni pamoja na kupaka rangi katika majengo ya umma kama vile hospital na zahanati na kukarabati majengo ya shule.

Pia amesema katika maadhimisho hayo kutaendeshwa maonesho ya ubunifu na teknolojia pamoja na maonesho ya ujuzi pamoja na kutoa vyeti vya heshima Kwa watu mbalimbali kutokana na mchango wao katika shughuli za maendeleo na mafunzo na ufundi stadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here