Home KITAIFA DK.MWINYI: ZANZIBAR ITAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA ROMANIA

DK.MWINYI: ZANZIBAR ITAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA ROMANIA

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuimarisha ushirikiano na Romania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kiuchumi.

Rais Mwinyi ametoa Tamko hilo leo Februari, 14 2025 alipozungumza na Balozi wa Romania nchini Tanzania Gentiana Serbu aliyefika Ikulu kuonana naye.

Ameeleza kuwa Uhusiano mzuri na wa muda Mrefu baina ya nchi hizo mbili unapaswa kuimarishwa zaidi kwa kufungua milango zaidi ya Ushirikiano na kufanya kazi kwa Ukaribu katika sekta mbalimbali
za Maendeleo.

Dk. Mwinyi amemuelezea Balozi Gentiana kuwa yapo Maeneo mengi ambayo nchi hizo zinaweza kushirikiana ikiwemo elimu , Afya, mafuta na gesi , usimamizi wa maafa na udhibiti wa taka kitaalamu pamoja na mawasiliano na teknolojia ya habari.

Akizungumzia suala la mazingira Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa Zanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa la taka za plastiki zinazotishia uhai wa viumbe vya baharini na ustawi wa sekta ya utalii na kuiomba Romania kulizingatia eneo hilo.

Akizungumzia sekta ya elimu amevikaribisha Vyuo Vikuu vya Romania kuja nchini kuangalia maeneo ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Aidha ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Romania kuja kuangalia fursa za uwekezaji hapa nchini.

Naye Balozi Gentiana Serbu ameihakikishia Zanzibar kuwa nchi hiyo itaendelea Kushirikiana nayo na kutoa Misaada katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuleta Maendeleo na Ustawi wa Watu wake.

Balozi Gentiana ameyataja maeneo ambayo nchi yake inalenga katika ushirikiano na Zanzibar kuwa ni usimamizi wa maafa, Elimu ,afya teknolojia ya mawasiliano ,uwekezaji na maendeleo ya viwanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here