Home KITAIFA TUICO YAWATAKA WANACHAMA WAKE KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI

TUICO YAWATAKA WANACHAMA WAKE KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI

Esther Mnyika @Lajiji Digital

CHAMA Cha Wafanyakazi  wa Viwanda, Biashara,Taasisi za Fedha Huduma na Ushauri (TUICO) kimewataka wanachama wake kujipanga katika kugombea na kuchagua viongozi wa wa chama hicho watakaolinda uhai  na maslahi ya chama.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari, 10 2025 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa TUICO Paul Sangeze wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa hali bora kati ya TUICO na mwajiri na TUICO na chama Cha wafanyakazi.

Amesema  wanachama wa chama hicho wanategemea kufanya uchaguzi ndani ya mwaka huu ambapo wametakiwa kuacha kupitisha viongozi bila kupingwa kwakuwa uchaguzi wa aina hiyo hauleti viongozi wazuri.

“Mwaka huu 2025  ni mwaka wa uchaguzi wa chama chetu cha TUICO,ninawaomba kila mmoja wetu katika nafasi yake kuhakikisha chama kinapata viongozi bora watakaolinda uhai wa chama.

“Hakikisheni kuwa kanuni,masharti na utaratibu wa chama unafuatwa  kusiwe na kupitisha kaa viongozi bila kupingwa hata kama mgombea ni mmoja utaratibu wa kura ufuatwe yaani kuwa na Ndiyo au  Hapana kila mmoja asisahau kumwamba Mwenyezi Mungu  tuwezw kuvuka salama,”amesema  Sangeze.

Amesema pia ni wajibu wa kila mmoja na watendaji  wote wa chama kuhakikisha  wanakilinda chama dhidi ya maadui wasiokitakia mema chama.

Akizungumza kuhusu mafanikio alisema katika kipindi  cha mwaka mmoja  chama kimeweza kupata wachama wapya 15,032,kufunga mikataba  ya hali bora 98.

Amesema migogoro 303 ilipokelewa  ambapo kati ya hiyo na migogoro 214 ilishinda huku kamati 108 za majadiliano ziliundwa.

Amesema ziara  3166 zilifanyika ,mikutano 44,854 uliofanyika ,semina 44,150 huku wafanyakazi bora 182 walipata zawadi.

Naye Mkuu Sekta ya Biashara TUICO Makao Makuu, Willy Kibona amesema mkataba huo kuboresha Masalahi  na kuwasaidie wafanyakazi wanachama na wenye tija.

“Baadhi ya mambo ambayo yapo kwenye mkataba huu mfanyakazi akipata madhara au msiba kwa watu husika  mwajiri kugharamia,”amesema Kibona.

Kwa upende wake Katibu  Msaidizi TUICO Kigamboni, Hamisa Simba Alisema Mkataba huo ukawe chachu na tija kwa kila mfanyakazi na mahala pakazi hakikisheni wanakuwa na mshikamano wa pamoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here