Home AFYA TAMA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI,UNFPA NA CHAMA CHA WAKUNGA CANADA WAMEANDAA MAFUNZO...

TAMA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI,UNFPA NA CHAMA CHA WAKUNGA CANADA WAMEANDAA MAFUNZO MAALUM YA HUDUMA ZA DHARULA KWA WAKUNGA

Na Esther Mnyika, @lajiji.co.tz

CHAMA Cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na serikali ,UNFPA na Chama cha Wakunga Canada wameanda mafunzo maalumu ya huduma za dharula kwa wakunga pindi wanapowahudumia wakinamama wanaojifungua kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya vinavyotokana wakati wakujifungua.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Dk.Beatrice Mwilike

Mafunzo hayo ambayo yapo chini ya Mradi wa mradi wa thamini uzazi salama wenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za dharura kwenye wakunga kwenye vituo vyao.

Akizungumzaleo Februari, 10 2025 jijini Dar es Salaam Rais wa TAMA, Dk.Beatrice Mwilike wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tano yameanza Salaam yanatolewa kwa awamu ambapo kwa kundi la kwanza jumla ya wakunga 30 huku kundi lingine la wakunga litapata mafunzo hayo siku 10 zijazo ambapo jumla itakuwa siku 15,matarajio ni kuwafikia wakunga 90 wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya vya kutolea huduma za afya.

Amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo wanawake wakati wakujifungua ni kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo mafunzo hayo yatamjengea mkunga kukabiliana na changamoto hiyo.

“Mafunzo hayo tunaangalia je wakunga wanaweza vipi kumsaidia mama anayepoteta damu kipindi ambacho ni mjamzito kabla hajajifungua ,pia tunatoa mafunzo kwenye kuangalia ni namna gani wakati wa uzazi pengine mama anataka kujifungua mabega yamenasa ni namna gani tutamsaidia hivyo tunawaelekeza ni namna gani ya kufanya kuweza kumsaidia lakini pia kuna ile mama ameshindwa kujifungua kawaida kuna namna yakuweza kumsaidia mama huyo hivyo mafunzo haya yote yatawasaidia wakunga hawa,”amesema Dk.Beatrice.

Kwa upande wake Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto Dar es salaam, Agness Mgaya amesema changamoto zipo nyingi katika kuhudumia mama mjamzito pamoja na kichanga na hasa pale dharura inapokuwa inajitokeza hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuwapa uelewa zaidi.

“Tunajua kuwa tunafanya vizuri kuwahudumia hawa wajawazito na watoto wachanga lakini lazima kila wakati tuwape watu elimu kwani kutoa huduma ya afya ni sayansi na sayansi inakuwa inabadilika kila siku kwaiyo pale ambapo panakuwa na maboresho lazima na sisi wakunga wetu wasiachwe nyuma waweze kujengewa uwezo na kukumbushwa nini ambacho kinapaswa kufanyika,”amesema.

Ameongeza bado wanachangamoto kubwa sana kwenye ushiriki wa wenza kwenye huduma za afya uzazi na mtoto wanaume wamekuwa wapo mbali kuwasindikiza wake zao.

Ametoa wito wanaume waweze kuwasindikiza wake zao wanapoenda kupata huduma za afya ya uzazi mama anapokuwa mjamzito lakini pia wakati mama anapojifungua wamsindikize inamsaidia sana mama kupata moyo kwamba yupo na mwenzake na kumpunguzia maumivu.

Amesema asilimia 47 ya wanaume ndio wanashiriki kwenye huduma za afya ya uzazi na mtoto.

Nao wakunga walioshiriki mafunzo hayo Paul Zakaria na Sarah Hallan wamesema mafunzo hayo watakayoyapata itawajengea uwezo na watatuwa kipaumbele kwa wengine pindi warudipo kwenye vituo vyao vya kazi.

Mradi huo wa mafunzo ya thamini uzazi salama ni wa miaka saba na unatekelezeka kwa mkoa wa Dar es salaam na Shinganga kwani vifo vya Mama na mtoto kwenye mikoa hiyo imeonekana ni kinara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here