Home SIASA RAIS DK. SAMIA : CCM NDIO CHAMA KIKUBWA LAKINI BADO HAWAPASWI...

RAIS DK. SAMIA : CCM NDIO CHAMA KIKUBWA LAKINI BADO HAWAPASWI KUBWETEKA

DODOMA 

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kazi kubwa iliyofanywa na Chama chicho wananchi bado wana imani nacho na kuwapa dhamana tena ya kuongoza Serikali zote mbili na CCM ndio Chama kikubwa lakini bado hawapaswi kubweteka.

Rais Dk. Samia ameyasema hayo mapema Leo Februari 5, 2025 jijini Dodoma katika Maadhimisho ya miaka 48 ya Kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi amesema wasiruhusu kunyemelewa na kibri cha kubeza wapinzani wao na wasiruhusu kuingiwa na pepo la kuwaogopa watu hao.

“Tukiangalia kazi tuliyoifanya katika kipindi hiki naamini kuwa uchaguzi wa mwaka huu 2025 hali haitakuwa tofauti kwani Watanzania wataendelea kutupa dhamana ya kuongoza Serikali zote mbili yani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Lakini pamoja na kazi hiyo Tusibweteke,ndugu zangu pamoja na kazi hiyo ya kujiamini na kwamba CCM ndio Chama kikubwa na tuna matumaini makubwa katika uchaguzi ujao tusibweteke. Kama nilivyosema katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliopita hivi karibuni,tusiruhusu kunyemelewa na kibri cha kuwabeza wapinzani wetu lakini pia tusiingiwe na pepo la kuwaogopa,”amesema.

Aidha Dk.Samia amendelea kusisitiza kulinda heshima na imani waliyopewa na Wananchi katika kuliongoza Taifa hasa katika kipindi wanapoadhimisha uhai wa Chama hicho.

“Tuendelee kulinda heshima na Imani tuliyopewa na Wananchi ya kuliongoza Taifa letu, na tunapoadhimisha miaka 48 ya uhai wa chama chetu tuwahakikishie Wananchi kuwa CCM imejipanga kuendelea kutoa uongozi thabiti kwa Ustawi wa Taifa letu,”amesema.

Pia amegusia mikakati ya serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuvutia uhitaji wa uwekezaji na vijana wa kitanzania kuweza kunufaika.

“Serikali imeweka program na mipango mbalimbali ya kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuvutia uhitaji zaidi wa uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi iki vijana wetu waweze kujiajiri na kuajiriwa kupitia mazingira hayo bora ya biashara,”amesema.

Maadhimisho haya ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi yamehudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here