Dodoma
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Dodoma kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 48 ya Kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi .
Alipowasili leo Februari, 4 2025 Uwanja wa Ndege wa Dodoma Dk.Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt, Mohamed Said Dimwa.
Kilele cha Sherehe hizo zitafanyika kesho tarehe 05 Februari 2025 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.