Home KITAIFA WAJITEKA NA KUDAI PESA KUTOKA KWA WAZAZI WAO

WAJITEKA NA KUDAI PESA KUTOKA KWA WAZAZI WAO

Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata wasichana wawili kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 04, 2024, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa Januari 29, mwaka huu, Jeshi hilo liliwapata na kuwahoji wasichana wawili mwanafunzi wa Kidato cha Pili (16) na mwingine Mwanafunzi wa Darasa la saba (12) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es salaam.

Amesema wasichana hao wamekamatwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.

“Jeshi linalaani vitendo hivyo vya watu vyenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu,” amesema.

“Ufuatiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubaini watoto hao walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hilo la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka Januari 26, 2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi Januari 27, mwaka huu asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipokamatwa wakiwa wakizunguka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here