Home SIASA WASIRA: UAMUZI WA MKUTANO MKUU UMEZINGATIA KATIBA YA CCM

WASIRA: UAMUZI WA MKUTANO MKUU UMEZINGATIA KATIBA YA CCM

Awapa darasa wanaodai sababu ya CCM kupitisha wagombea Urais

Asema yupo tayari kuwapa somo waifahamu vyema katiba ya Chama Β 

Dar es Salaam

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mainduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliomchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kugombea kiti cha Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umezingatia takwa la kikatiba na mamlaka ya Mkutano Mkuu.

Wasira ameyasema hayo leo Januari, 26 2025 jijini Dar es Salaam wakati viongozi, wanachama, Β wapenzi wa CCM na wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipojitokeza kumpokea.

Amesema baadhi ya watu wanaojiita wanaCCM wanaodai kwamba bado hawajaelewa sababu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupitisha uamuzi huo, atawasaidia kuelewesha kwani uwezo wa binadamu kufahamu jambo hauwezi kulingana.

“Baada ya Mkutano Mkuu kutambua kazi kubwa zilizofanywa na serikali zote mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, Mkutano Mkuu wa CCM ukasema kama hali ni hii kuna sababu gani kuchelewesha kutangaza mgombea?.

Sasa wapo watu wanaosema wao ni wanachama wa CCM, hawakuelewa. Hilo nalo siyo jambo la ajabu. Tutawasaidia kuelewa maana siyo watu wote wanaweza kuelewa sawa. lakini tunawaambia Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo kikao kikuu cha mwisho,” amesema.

Wasira ameeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Chama una mamlaka ya kubadili, kufuta na kurekebisha uamuzi wowote uliofanywa na kikao cha chini yake, kufuta maamuzi yaliyofanywa na kiongozi yeyote wa CCM.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here