Dar es salaam
WILAYA ya Ubungo inamkakati wa kuhakikisha masoko, stendi na maeneo ya kimkakati na huduma za kijamii zinapatikana masaa 24 na zinafata uhakika wa mwanga wa kutosha katika maeneo yote.
Akizungumza Januari, 24 2025 jijini Dar es salaam Mkuu wa wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko(ambaye amehamishiwa katika wilaya ya Hai)wakati akizindua kampeni ya ‘usiku kama mchana’ kwenye kikao kilichohudhuliwa na wenyeviti na watendaji wa mitaa yote 90 ya ya wilaya hiyo.
Amesema wamejipanga kuanza biashara kwa saa 24 kwa kuimarisha miundombinu ya ufanyaji wa biashara hizo ikiwemo kufunga taa za barabarani na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama.
“Ajenda hii tumeamua kuibeba kwa sababu ya wilaya yetu ya Ubungo ni eneo la kimakakati ni eneo ambalo ndio lango la jiji na ni eneo ambalo ni linanafasi kubwa sana katika biashara za mkoa wetu wa Dar es Salaam, tunayo masoko makubwa ya kimkakati tunazo stendi kubwa za mabasi na daladala na tunayo masoko,” amesema Bomboko
Ameeleza kuwa maeneo hayo mhimu yanawafanya waweze kuangali namna watu wanaweza kufanya biashara kwa masaa 24.
Amesema kuwa kunamambo ya msingi yanatakiwa yafanyike ili biashara na shughuli za uzalishaji ziwe,e kufanyika kwa ufanisi zaidi.
Amesema Ulinzi na usalama lazima uimarishwe na kuhakikisha kuwa wanatoa mazingira mazuri kwa wafanyabiashara kuwa na uhakika wa usalama wa mali zao na wao wenyewe.
Ameeleza kuwa wamehakikisha huduma zote mhimu zinaendelea kutolewa kwa saa 24 hii ni pamoja na huduma za afya, huduma nyingine za kijamii, kama maji na umeme upatikane kwa uhakika kwa saa zote 24 lakini pia kuwa na uhakika wa miundombinu kama barabara ziwe zinazofikika katika maeneo yote ya wilaya ya ubingo na kuwa na taa za barabarani zinazotoa mwanga ili ziweze kutafsiri kazi zinazofanywa usiku na mchana.
“Usiku ili uwe mchana ni lazima kuwe na mwanga watu wanapofanya kazi lakini pia ulinzi na usalama lazima uzingatiwe,”amesema.
Akizungunzia maandalizi ya kampeni ya Usiku kama Mchana, Bomboko amesema yameshakamilika kwa asilimia 80, ndio maana wameanza kutoa taarifa kwa umma, na asilimia zilizobaki wanaendelea kuimarisha miundombinu ili kufanikisha kampeni hiyo kwa saa 24.
Amesema kuwa masoko yaliyoainishwa ni Soko la Mahakama ya Ndizi, mabibo, Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi, kituo cha daladala cha Mbezi mwisho na Soko la Kuchinja kuku la Shekilango, Manzese Baharesa, Sinza na Mlimani City.
Amesema kuwa asilimia hizo zilizobaki wanaendelea kuonesha maeneo muhimu kama msigani Maramba, soko la Kwa Beda na Mburahati.
Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alishatangaza kuwa Soko la Kariakoo wataanza kufanyabiashara kwa saa 24 za wiki.