Dodoma
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mgombea urais, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Rais Dk.Samia amesema Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike umakamu wa rais baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo lakini kwa sasa Dk. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.
Akizungumza leo Januari kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM jijini Dodoma Dk. Samia amesema Dk.Nchimbi ataendelea kuwa katibu Mkuu wa Chama hicho hadi Uchaguzi Mkuu utapokaofanyika.
Balozi Dk.Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari, 15.2024 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama kilichofanyika Unguja Visiwani Zanzibar.
Nchimbi alichukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba, 29 mwaka 2023.