Home Uncategorized RAIS DK.SAMIA NA DK.MWINYI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

RAIS DK.SAMIA NA DK.MWINYI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutekeleza azimio la Mkutano Mkuu kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kikao kilichofanyika leo Januari, 19 2025 katika ukumbi wa NEC maarufu kama White House ambapo Wajumbe wamepitisha jina la Dk. Samia Suluhu Hassan kwa upande Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here