Home Uncategorized RAIS DK.SAMIA AKEMEA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

RAIS DK.SAMIA AKEMEA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Dodoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,amekemea baadhi ya wanachama wa CCM wenye tabia ya kuendeleza makundi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu badala ya kuwaunga mkono wagombea waliopitishwa na Chama.

Rais Samia ametoa onyo hilo leo Januari 18,2025 wakati akizungumza na maelfu ya wajumbe, viongozi wakuu, wastaafu, mabalozi na wageni kutoka vyama rafiki wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jijini Dodoma.

Amesema kuwa wapo baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakiendeleza makundi ya uchaguzi licha ya Chama kupitisha jina la mgombea.

“Teueni wagombea wanaokubalika na kutounda makundi, tunasema makundi ndani ya Chama wakati wa kuomba ni kwa sababu ya demokrasia kwani waombaji ni wengi hivyo tutapata makundi. Lakini tutakaposimamisha wagombea wa Chama chetu tunaomba makundi yasiendelee,” amesema.

Rais Dk. Samia ameongeza  kuwa katika mwaka huu wa uchaguzi, wanachama wanawajibika kuendelea kuwa wamoja zaidi katika kukamilisha ushindi wa CCM kwani maendeleo ya nchi yapo mikononi mwa CCM.

Aidha ametoa wito wa kutodharu vyama vya upinzani au kuingia uwoga dhidi ya vyama hivyo kwani lazima CCM kipambane kulinda heshima ya wananchi ambao wameendelea kukiamini kwa miaka mingi.

“Maendeleo ya nchi yapo mikononi mwa CCM, tusiruhusu kunyemelewa na kiburi cha kuwadharau wapinzani wetu, tusiingie pepo la kuwaogopa tupambane nao ili kulinda heshima ya wananchi waliotukabidhi,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine Dk.Samia ametoa onyo kwa wanachama wa CCM wenye nia ya kugombea nafasi za ubunge na udiwani ambao wameanza kampeni za mapema kabla ya wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here