Home AFYA RADIAN LIMITED YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA MAHITAJI YA KIJAMII KWA...

RADIAN LIMITED YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA MAHITAJI YA KIJAMII KWA WAGONJWA MOI

Dar es Salaam

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Radian Limited kupitia kitengo chake cha Radian for Development limetoa msaada wa vifaa tiba, mahitaji ya kijami na kulipia gharama za matibabu kwa watoto watatu wenye vichwa vikubwa wanaopatiwa huduma za matibabu MOI.

Akikabidhi msaada huo leo Ijumaa Januari, 17 2025 Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kitengo cha Radian for Development, Aneth Sokombi amesema kuwa wametoa vifaa tiba, mahitaji ya kijamii yakiwemo Nepi, sabuni za kufulia, taulo za kike na wamelipia gharama za huduma za matibabu ya watoto watatu.

Ameongeza kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kugusa jamii na kurudisha tabasamu la wagonjwa hao.

“Leo tumeweza kutembelea hapa hospitalini (MOI) tumeleta msaada wa vifaa tiba, mahitaji ya kijamii (sabuni, nepi, taulo za kike/pedi) na tumelipia gharama za huduma za matibabu kwa watoto watatu wenye changamoto ya vichwa vikubwa,”amesema Aneth.

Akipokea msaada huo Meneja wa Ustawi wa Jamii na Tiba Lishe wa MOI, Jumaa Almasi amelishukuru shirika hilo kwa kwa kujali wagonjwa wenye uhitaji na ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kutoa msaada kwani mahitaji ni makubwa.

“Kwanza tunawashukuru sana Radian kwa msaada wao, na muendelee kuwa na moyo huo, naomba nitoe wito kwa wadau wengine waweze kujitokeza kutoa msaada maana mahitaji ni makubwa,” amesema Almasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here