Home KITAIFA DOROTHY SEMU ATANGAZA KUGOMBEA 2025

DOROTHY SEMU ATANGAZA KUGOMBEA 2025

Dar es Salaam

KIONGOZI wa Chama cha ACT –Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16, 2025, jijini Dar es Salaam Dorothy amesema hatua hiyo imesukumwa na mambo manne ambayo ameyaona kama mapungufu.

“Nimejipima na nimeona ninatosha, nimekuwa kiongozi kwenye nafasi mbalimbali hata kabla ya kuingia kwenye siasa, pia ni kiongozi wa chama bora, chenye sera na ilani bora,” amesema Semu.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni, kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, changamoto ya ajira kwa vijana na udhaifu katika usimamizi wa rasilimali za taifa.

“Nimeona kuwa Tanzania inahitaji kiongozi mpya anayeweza kubadilisha hali ya maisha ya watanzania pamoja na uchumi wa nchi hivyo nipo tayari kuchuana na vyama vingine vyote endapo chama changu cha ACT Wazalendo kitanipa ridhaa,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here