Home KITAIFA WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO.

WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO.

Msumbiji

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025.

Chapo alishinda Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, 2024.

Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.

Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa Independence (Uhuru) jijini Maputo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here