Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu amemweleza Fujii kuwa Tanzania imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kufanya uwekezaji ambayo yanawawezesha wawekezaji kunufaika na shughuli zao.