Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella, amemtembelea kwa ajili ya kumsabahi na kumjulia hali Mzee Philip Japhet Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), nyumbani kwake Msalato, Dodoma, leo Jumapili Januari, 12 2025. Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye maktaba ya Mzee Mangula, Balozi Nchimbi pia alipata wasaa wa kuchukua picha yeye mwenyewe kwa njia ya ‘selfie’, kama inavyoonekana pichani.