Home KIMATAIFA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI AFRIKA WAIPA KONGOLE TANZANIA UZALISHAJI MAZAO YA...

WAKUU WA NCHI NA SERIKALI AFRIKA WAIPA KONGOLE TANZANIA UZALISHAJI MAZAO YA CHAKULA AFRIKA.

*Rais Museveni asifu bora wa mchele wa Tanzania, asisitiza kushindana kwa ubora

Uganda

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa nchi za Afrika wameonesha matumaini makubwa na mikakati iliyowekwa na Tanzania katika kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora hasa mpunga na mahindi.

Ameyasema hayo leo Jumamosi, Januari 11, 2025)alipomwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika wa kupitisha Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 – 2035) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala nchini Uganda.

Majaliwa amewahakikishia Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha masuala ya utafiti na kushirikisha sekta binafsi, taasisi za umma zinazojishughulisha na kilimo ili kuhakikisha nchi inakuwa tegemeo katika uzalishaji wa chakula barani Afrika.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imefarijika kusikia baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika akiwemo Mheshimiwa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakiisifia Tanzania kwa kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora na hasa mpunga na mahindi. “Haya ni mafanikio makubwa katika kta ya kilimonchini,”

“Natamani watu washindane kwa ubora katika uzalishaji, mfano mchele wa kutoka Tanzania ni bora zaidi na gharama yake ipo chini, kuna wakati walitaka nizuie usije lakini nikawataka nao wajitahidi kushindana katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora.” Kauli ya Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni aliyoitoa wakati akiwasilisha hotuba yake katika mkutano huo, inatoa fursa kwa mataifa mengine kununua mchele kutoka Tanzania.

Majaliwa amesema kuwa Tanzania imeweka mkakati wa kuhakikisha inaendelea kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani na kuuza  ziada nje. “Kwa sasa kilimo chetu si cha kujikimu bali ni cha kibiashara.”

Awali, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza ili kuongeza tija na kukuza ajira hususan kwa vijana.

Ametoa mfano wa zao la kahawa, ambapo nchini Uganda kilo moja ya kahawa ghafi inauzwa dola mbili za Marekani, ambapo kahawa hiyo hiyo ikichakatwa bei inaongezeka na kuuzwa dola 40 za Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here