Na Boniface Gideon, Handeni
WATU 8 wamefariki Dunia Wilayani Handeni mkoani Tanga, baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso Lori na Coaster katika Kitongoji cha Kwachuma Kata ya Segera.
Taarifa iliyotolewa naJeshi la Polisi iliyomnukuu Kamanda wa Polisi ACP. Almachius Muchunguzi imeeleza kuwa ajari hiyo imetokea Disemba 24 2024 majira ya saa 11:00 Alfajiri.
Gari lenye Usajili wa T780DRL Lori ,aina ya Sharkman likiwa na tela lenye Usajili wa T692 ESH mali ya kampuni ya Starling Gulf Trading Company, likitokea Jijini Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam,liligongana na gari aina ya Toyota Coaster yenye Usajili T 706DPJ,likitokea Jijini Dar es salaam kwenda mkoani Kilimanjaro.
“Katika ajari hiyo,vifo vya watu 8 kati yao Wanaume wapo 5 na wanawake 5 na majeruhi 8 wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Korogwe Magunga,huku Maiti zikihifadhiwa katika chamba cha Maiti katika hospitali hiyo” imeeleza taarifa hiyo
Kamanda Muchunguzi ameeleza kuwa ,chanzo cha ajari hiyo ni Dereva wa gari aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda mkoani Kilimanjaro kushindwa kulimudu kutokana na kutembea kwa mwendo mkali,hali iliyosababisha kutokea kwa ajari hiyo mbaya zaidi.
“Chanzo cha ajari hiyo, ni Dereva wa gari aina ya Toyota Coaster kushindwa kulimudu kutokana na kutembea kwa mwendo mkali,niwatake madereva wote kuzingatia Sheria za Barabarani,hatutasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayevunja Sheria za usalama Barabarani,na tupo chonjo saa 24 ,hivyo atakayekiuka Sheria za usalama Barabarani tutamchukulia hatua Kali za kisheria,” ameeleza Afande Muchunguzi.