Home KITAIFA WAZIRI KIKWETE: SERIKALI ITAWEKA SERA MADHUBUTI INAYOTOA MUONGOZO UNAOSIMAMIWA IPASAVYO

WAZIRI KIKWETE: SERIKALI ITAWEKA SERA MADHUBUTI INAYOTOA MUONGOZO UNAOSIMAMIWA IPASAVYO

Dar es Salaam

SERIKALI imesema itahakikisha inaweka sera madhubuti inayotoa muongozo unaosimamiwa ipasavyo kwa ajili ya kuwainua  vijana na kuboresha uwekezaji wa Startups nchini kwani hao ndio injini chipukizi ya maendeleo na uchumi wa nchi.

Haya yameelezwa leo Disemba, 20 2024 jijini Dar na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (kazi vijana ,ajira na wenye ulemavu ), Ridhiwan Kikwete wakati akifunga wiki ya makampuni bunifu (Startup) lililofanyika wiki nzima katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema lengo ni kutengeneza uchumi unaojitegemea na uchumi wa kiteknolojia.

Amesema serikali,sekta binafsi na wadau wa maendeleo watahakikisha wanashirikiana na waweze kukua kwa haraka na kuwa sehemu ya maendeleo ya uchumi wa nchi huku kampuni binafsi  zinakuza ajira kwa vijana.

“Wizara itahakikisha inatengeneza mazingira mazuri ya Startup kukua kwani Startup ni sehemu ya biashara zinazolenga kukua kwa haraka zaidi kwa kutumia bunifu mpya na za kiteknolojia kwa kuleta suluhisho jipya,na kwa haraka zaidi,” amesema.

Kikwete amesema  duniani ya leo ni ushindani  hivyo Tanzania  ili ziweze kukuza Startups lazima kuweka mazingira mazuri ya kisera na kanuni na ni jukumu lao.

Ameongeza kuwa kongamano hilo lilitoa nafasi  kwa wabunifu kuonesha bidhaa zao na kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu. 

“Haya ni mafanikio makubwa  ya kutengeneza mazingira mepesi kwa vijana  kutengeneza mitaji na kupata vyanzo vya kuendesha maisha yao ya kila siku,”amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Startup Association, Zahoro Muhaji amesema kuwa Tamasha hilo limekua na mafanikio  makubwa na kwamba  Startups imekua ikichangia pato la taifa  ajira ambapo kwa miaka minne tangu kuanza kwa Startups nchini imeweza kuchangia uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni tatu  na ajira na kazi 10,0000 mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here