Dar es Salaam
ALIYEWAHI kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kuanzia mwaka 2001 hadi 2013 Jaji John Tendwa amefariki dunia.
Taarifa hiyo imetolewa leo Disemba,17, 2024 jijini Dar es Salaam na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amesema Jaji Tendwa amefariki dunia leo Disemba, 17 katika Hospitali ya Taifa Mhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Amesema taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na familia kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili.
Amesema Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kibamba Hospitali, ratiba na taarifa rasmi za mazishi zitatolewa mara baada ya kukamilika.