Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA TUME YA MABORESHO YA KODI

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA TUME YA MABORESHO YA KODI

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana leo Disemba,16 2024 na Tume ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Zanzibar iliyofika kujitambulisha.

Katika maongezi na Tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dk. Mwinyi wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayozishauri Serikali mbili za SMZ na SMT kuhusu masuala ya kodi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuteua Tume hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuimarisha na kubadilisha mifumo ya kodi kwa Serikali zote mbili za SMZ na SMT, itakayoleta mageuzi kwenye biashara likiwemo eneo la kodi hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake Balozi Sefue amezishukuru Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuahidi ushirikiano na Tume hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here