Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameshiriki hafla ya uwekaji Wakfu Jengo la Kanisa la Waadventista wa Sabato Magomeni inayofanyika leo Disemba 15, 2024 jijini Dar es Salaam.
Dk. Biteko amemwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo Kanisa hilo limewekwa Wakfu na Mchungaji Joel Okindo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD).